HOME BARUA YA WAZI KWA AKINA MKAPA
Enyi Washenzi Makatili 

Dikteta Benjamini Mkapa,

Chinjachinja Omari Ali Juma,

Dikteta Amani Karume,

Frederic Sumaye,

Omari Mahita,

Wajumbe wote wa kabinet ya mauwaji,

Na wafuasi wenu wote watiifu,

Natumai nyote muko katika hali ya furaha sana hasa baada ya kupata ushindi mkubwa sana katika vita vyenu dhihi ya raia wa Zanzibar wasio na hatia. Wananchi wote tumeona jinsi gani upeo wa busara zenu munazotumia katika kuendesha nchi. Pia tumeona ukweli wa yale maneno yenu ya 'uwazi, amani na utulivu'.

Mshenzi Mkapa. Kuna msemo kuwa "Mmakonde hamli nduguye". Nasi kwa kujua kuwa una asili ya pande za kule kusini, bila ya shaka kwako wewe kuchinja sio jambo geni sana, au hata labda nawe ni miongoni wa wanaokula watu. Hatutoona ajabu kusikia ulituma watu kwenda kuwinda Zanzibar, nawe ukawekewa fungu lako kutokana na mawindo hayo, upitishie mvinyo ulioleta kutoka huko safarini ulikokuwa.

Chinjachinja Omri Ali Juma. Ukweli umejitokeza kuwa "Mchawi hutoa mtu wake". Wazanzibari hatutashangaa kusikia sasa umerithisha kile kiti cha uchawini alichokiacha baba yako. Usifikiri tumesahahu kuwa baba yako alipokuwa taabani kitandani ulimkimbia  kwa tuhuma za kuwa mchawi mkuu. Nawe jitayarishe kukimbiwa kwani tayari sifa zote za kuitwa mchawi unazo, si tu na familia yako bali na Wazanzibri wote wenye akili timamu, kwani wewe ndie miongoni mwa waliotoa jeshi kwenda kuuwa watu ovyo.

Mshenzi Amani. Uraisi wako haukuhitaji watabiri maarufu kujua nini utakifanya. Mwana wa nyoka ni nyoka. Kama alivyokuwa mzee wako kibaraka wa Tanganyika ndivyo ulivyo wewe. Kama alivyokuwa dikteta ndivyo ulivyo wewe. Kama alivyokuwa katili ndivyo ulivyo wewe. Kama alivyokuwa mbakaji ndivyo ulivyo wewe. Nini tena la ajabu kwetu? Lakini wewe ndie unaejua zaidi kuliko mwengine yoyote juso la baba yako lilivyokuwa siku ya kifo chake.

Mshenzi Omari Mahita. Tunajua jinsi gani ulivyo mtiifu kwa viongozi wako, unapokea amri zote mbaya na kuongeza utakayo mwenyewe. Amri yako ya kuuwa labda ndiyo inakupandisha vyeo na mishahara. Endelea na kazi yako, kula kunywa ukicheka. Jua tu mikono yako ina damu nyingi sana.

Washenzi Mapuri, Khatibu, Sumaye,  na wenzenu wote katika kabinet ya mauwaji. Kamwe nanyi hatutowasahau katika maisha yetu.

Namalizia barua hii kwa salamu zangu kemkem kwa hao mapolisi wenu wapenzi na watiifu.

Mzanzibari Mwenye Uchungu..

 

 

 

HOME